Vitu 5 vya Kuangalia Kabla ya Ku-hire Developer
Imesasishwa: Julai 2026
Kuajiri developer asiyefaa kunaweza kugharimu muda, pesa, na hata sifa ya biashara yako. Kabla ya kumwajiri mtu yeyote, hakikisha unaangalia vitu hivi vitano.
1. Portfolio Halisi
Muombe aonyeshe kazi alizowahi kufanya — websites, apps, au systems halisi zinazofanya kazi, si screenshots pekee.
2. Uthibitisho wa Utambulisho
Hakikisha unajua jina lake halisi, mawasiliano yake, na mahali alipo. Hii inapunguza hatari ya kupotelewa na pesa au mradi wako.
3. Uwazi wa Bei na Muda
Developer mzuri atakupa makadirio wazi ya gharama na muda wa kukamilisha mradi kabla ya kuanza kazi — si ahadi zisizo na msingi.
4. Mawasiliano Mazuri
Angalia jinsi anavyojibu maswali yako mapema — hii ni kiashiria kizuri cha jinsi atakavyokuwa wakati wa mradi halisi.
5. Maoni Kutoka kwa Wateja Wengine
Kama inawezekana, ongea na mteja mwingine aliyewahi kufanya naye kazi kujua uzoefu wao.
Hii ndiyo sababu KS Developer inafanya uthibitisho (verification) kwa kila developer kabla hujamfikia — ili wewe usilazimike kufanya uchunguzi huu wote peke yako.